Simba Yashuka Viwango CAF Ranking 2026, Yanga Yapanda. Klabu ya Simba Sports Club imeshuka katika viwango vya ubora wa vilabu barani Afrika vilivyotolewa na Confederation of African Football, kufuatia matokeo yasiyoridhisha katika msimu wa michuano ya kimataifa 2025/2026.

Simba Yashuka Viwango CAF Ranking 2026, Yanga Yapanda

Simba Yapoteza Nafasi CAF Ranking

Kwa mujibu wa viwango hivyo vipya, Simba imeshika nafasi ya 11 ikiwa na pointi 38, ikishuka kutoka nafasi ya tano iliyokuwa nayo mwaka 2025. Kushuka huko kunahusishwa moja kwa moja na mwenendo wa timu katika mashindano ya kimataifa msimu huu.

Katika CAF Champions League, Simba ilimaliza mkiani mwa Kundi D, ikiwa nyuma ya:

  • Stade Malien
  • EspĂ©rance Sportive de Tunis
  • Petro de Luanda

Matokeo hayo yalichangia kwa kiasi kikubwa kuporomoka kwa alama zake.

Simba Yashuka Viwango CAF Ranking 2026, Yanga Yapanda
Simba Yashuka Viwango CAF Ranking 2026, Yanga Yapanda

Yanga Yaendelea Kupanda

Wakati Simba ikishuka, Young Africans Sports Club imeendelea kuimarika kwa kupanda hadi nafasi ya 12 ikiwa na pointi 35.

Yanga imefanikiwa kupita vilabu kadhaa vikubwa barani Afrika, ikiwemo:

  • Wydad AC
  • ASEC Mimosas
  • Orlando Pirates
  • TP Mazembe

Hali hii inaonyesha ukuaji wa kiwango cha Yanga katika mashindano ya CAF.

Katika nafasi za juu, Mamelodi Sundowns wanaongoza viwango hivyo, wakionyesha ubora wao kwa kutinga fainali ya CAF Champions League dhidi ya AS FAR.

Kwa upande wa CAF Confederation Cup, fainali itawakutanisha USM Alger na Zamalek SC.

Kwa sasa, kocha huyo anaihudumu Raja CA.

Kwa upande wa Yanga, iliwahi kufika fainali ya CAF Confederation Cup msimu wa 2022/2023 chini ya kocha Nasreddine Nabi, lakini ilipoteza dhidi ya USM Alger.

Pendekezo la Mhariri:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *